Wednesday, January 3, 2018

Arsenal vs Chelsea mtoto hatumwi dukani leo


Hatumwi mtoto dukani, ndivyo unavyoweza kusema pale baadaye Arsenal watakapowakaribisha Chelsea katika dimba lao la nyumbani Emirates katika mchezo ambao kila Timu inahitaji kupata matokeo ili kuweza kujiimarisha kileleni mwa Ligi.

Lakini pamoja na kwamba anaonekana mnyonge kocha Arsene Wenger amekuwa mgumu sana mbele ya Chelsea, rekodi za michezo mitano iliyopita zinaonesha Wenger amewafunga Chelsea mara tatu.

Ukichukua michezo waliyokutana EPL, Arsenal bado wanaonekana watemi mbele ya Chelsea kwani wameshawafunga mara 19,Chelsea wakishinda mara 17 huku timu hizo zikienda suluhu mara 15.

Arsene Wenger anajiamini zaidi akikutana na The Blues na hata mechi walizokutana  katika michuano yote kiujumla bado Arsenal ni wababe wa Chelsea wakishinda michezo 75,Chelsea akishinda michezo 62 na suluhu 55.

Mchezo wa leo utakuwa mchezo wa 6 kwa Antonio Conte kukutana na Arsene Wenger katika mashindano yote kuanzia mwanzo wa msimu uliopita huku Conte akifanikiwa kumfunga Wenger mara moja.

Rekodi hazidanganyi na kwa taarifa tu ni kwamba Chelsea uwanja wa Emirates ndio uwanja ambao wameshinda mechi nyingi za ugenini (5) idadi ambayo ni wao na Man United tu waliowahi kupata ushindi kiasi hicho uwanjani hapo.

2011/2012 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Arsenal kutopoteza michezo yote miwili ya msimu wa EPL mbele ya Chelsea huku msimu wa mwaka 1999 ndio mara ya mwisho kwa Arsenal kucheza mechi mbili na Chelsea bila kuruhusu bao.

Pamoja na kwamba kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ana mabao 19 Emirates lakini yote hayo amewafungia Arsenal na hajawahi kufunga tena katika uwanja huo tangu aondoke.



No comments:

Post a Comment