Thursday, January 4, 2018

Baridi kali Marekani limesababisha vifo vya watu 11


Watabiri wa hali ya hewa wanasema hali itaendelea kuwa mbaya mashariki mwa Marekani, na tayari kumeanza kuwa na theluji jimbo la Florida.
Marekani kwa sasa inakumbwa na siku ya 10 ya viwango vya baridi ambavyo vimevunja rekodi majira ya sasa ya baridi.
Baridi kali ilianza wakati wa Krismas
Ice and snow cover branches near the brink of the Horseshoe Falls in Niagara Falls, Ontario, Canada
Idara ya Taifa ya Utabiri wa hali ya Hewa (NWS) imetahadharisha kwamba hewa baridi kutoka Arctic itaendelea kutandaza katika theluthi mbili ya maeneo ya mashariki mwa Marekani hadi mwishoni mwa wiki hii.
Hilo litasababisha wimbi la upepo baridi kama wa kimbunga.
Upepo huo unaweza kuwa na nguvu kiasi cha kung'oa miti na kuharibu majengo.
Watu 20 wafariki kutokana na baridi kali Ulaya
Nyoka atafuta 'joto' kwenye kiatu
Viwango vya joto kwa wastani Jumanne maeneo ya mashariki mwa Marekani vilifikia 9.1F (-12.7C) kwa mujibu wa CBS News.
Mji wa Boston ni miongoni mwa miji inayotarajiwa kuathirika pamoja na miji ya mbali kwa mfano Orlando jimbo la Florida.
Wakazi katika maeneo ya kaskazini mwa Florida, ukiwemo mji wa Tallahassee, wameshuhudia theluji kwa mara ya kwanza katika miongo mingi.
Wengi wamekuwa wakipiga picha wakicheza kwenye theluji.
Shule katika maeneo mengi zimefungwa.



No comments:

Post a Comment