Thursday, January 4, 2018

Australia yatakuwa kuwa muuzaji mkubwa wa zao la bangi


Serikali ya Australia imetangaza kwamba inapania kuwa mwuzaji mkubwa zaidi wa bangi ya kutumiwa kwa ajili ya matibabu duniani.
Taifa hilo linapanga kufanyia mabadiliko sheria zake na kujiunga na Canada na Uholnazi ambazo kwa sasa ndizo nchi pekee ambazo huuza bangi nje ya nchi.
Uruguay na Israel pia zina mipango sawa. Waziri wa Afya Greg Hunt amesema hatua hiyo itawasaidia pia wagonjwa nchini Australia.
Taifa hilo liliidhinisha matumizi ya bangi kwa sababu za kimtaibabu mwaka 2016.
Kampuni zashindania kukuza bangi Denmark
Kampuni ya bangi yaununua 'mji wa bangi' Marekani
Matumizi ya bangi sasa ni halali California
Muuza bangi angia kimakosa ndani ya gari la polisi
Matumizi ya bangi kwa ajili ya burudani bado ni haramu.
"Lengo letu liko wazi: kuwapa wakulima na wenye viwanda wa Australia nafasi bora zaidi katika kuwa wauzaji nambari moja wa bangi ya kutumiwa kwa sababu za kimatibabu duniani," Bw Hunt amesema.
Thamani ya jumla ya biashara ya bangi duniani huenda ikafikia $55bn (£40bn; A$70bn) kufikia mwaka 2025, kwa mujibu wa makadirio ya kampuni ya Marekani ya Grand View Research.
Mapema wiki hii, California ilikuwa jimbo kubwa zaidi la Marekani kuhalalisha matumizi ya bangi kwa ajili ya burudani.



No comments:

Post a Comment