Friday, January 5, 2018

Kessy aibukia Mapinduzi Cup



Beki wa kulia wa Yanga Hassan Ramadhani ‘Kessy’ ameifungia Yanga bao pekee kwenye mchezo wao wa pili wa Kundi B dhidi ya JKU katika mashindano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Kama unavyojua, Kessy hapati nafasi mara kwa mara kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga mbele ya Juma Abdul amepewa fursa ya kuanza katika mechi mbili mfululizo za Mapinduzi Cup.

Goli hilo limeipa Yanga pointi tatu na kufikisha pointi sita sawa na Singida United ambao wanaongoza Kundi B kwa wastani wa magoli.

No comments:

Post a Comment