Thursday, January 4, 2018

FULL VIDEO: BOT Yazichinja na kuzifutia leseni Benki 5


Benki kuu ya Tanzania imezifungia na kuzifutia leseni ya Biashara,  pamoja na kuzifilisi kwa maana ya kutofanya kazi kabisa Benki tano ikiwemo benki ya efatha kwa kutotimiza masharti yaliowekwa na benki kuu ya Tanzania.

Akizungumza Leo jijini dar es salaam Gavanna Wa benki kuu,  prof. Benno Ndullu ametoa taarifa hiyo wakati akianga na kumkabidhi nafasi yake alio nayo gavanna mpya Prof.  Florence luoga,  amesema benki hizo zilipewa muda Wa miaka ili kuongeza mtaji kufikia kiwango kipya ambapo muda Huo uliisha juni 2017 na muda huo kuongezwa hadi kufikia disemba 31, 2017.

Prof.  Ndullu amesema benki tano kati ya nane zilishindwa kuandaa na kuwasilisha benki kuu mpango mkakati unaokubalika Wa kuongeza mtaji na pia kuzifanya benki hizo kuwa endelevu kutokakana na kutotimiza matakwa ya kisheriaya kuwa na mtaji kamili na Wa kutosha hivyo imeamua kuzifunga na kusitisha shughuli za kibenki benki hizo Ni.
1. Covenant Bank for women (Tanzania) limited
2.Efatha Bank Limited
3. Njombe Community Bank Limited
4. Kagera Farmers Cooperative
5. Meru Community Bank Limited
Benki kuu pia imeiteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa mfilisi Wa benki hizo tano.

Pia Benki tatu kati ya nane hakikukidhi matakwa ya sheria zimewakilisha benki mpango mkakati unaokubalika Wa kuongeza mtaji na kuzifanya ziwe endelevu na zimepewa muda hadi juni 30, 2018 endapo hazitatimiza agizo hilo zitafingiwa na kufilisiwa benki hizo Ni
1. Kilimanjaro Cooperative Bank Limited
2. Tanzania women Bank Plc
3. Tandahimba Community Bank Limited
Benki kuu imewahakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana kayika mabenki kwa lengola kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.
ANGALIA FULL VIDEO HAPA NA USISAHAU KU SUBSCRIBE......................




No comments:

Post a Comment