Thursday, January 4, 2018

Wakala wa Majengo mbaroni kwa kushindwa kukarabati Shule



Meneja wa wakala wa Majengo TBA mkoa wa Kigoma Mhandisi Mgalla Mashaka amekamatwa na polisi akituhumiwa kushindwa kukarabati  shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi  wa nane mwaka jana.

Meneja huyo amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu,sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kufanya ukaguzi katika shule hiyo  ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo,mabweni,maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika ambapo Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga ameagiza kuundwa Tume kumchunguza meneja huyo.

Kwa upande wake Waziri Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea.

Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo.


No comments:

Post a Comment