Wednesday, January 3, 2018

Nahodha Simba awatoa hofu mashabiki


Mashabiki wa Simba hawaelewi kilichotokea huko Kisiwani Zanzibar na watani wao  Yanga wanafurahii, baada ya Wekundu hao kuanza mshindano ya Kombe la Mapinduzi kwa sare ya 1-1 na Mwenge ya Pemba, lakini, beki wa kikosi hicho, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema, watawashangaza watu.

Zimbwe ambaye pia ni nahodha wa Simba, amewawashia moto huo wale wote wanaowabeza akisema, watanyamaza tu na kwa msisitizo akawaambia Jamhuri ya Pemba  wajiandae kwa sababu wana machungu.

"Tumeanza mechi vibaya kwa sare inauma, lakini ninachopenda kuwaambia mashabiki wetu watulie ni

jambo la marekebisho, tumeona tulivyocheza na mwalimu ameona, tunaenda kufanyia kazi yale

mapungufu ili mechi ijayo turudi vizuri,"amesema Zimbwe Jr.

Akizungumzia mchezo huo,  Zimbwe amesema: "Tena wajiangalie kwa sababu tumefanya kosa mechi iliyopita, hivyo hatutaweza kurudia kosa ni ushindi."


No comments:

Post a Comment