Msanii wa muziki Bongo, Msamii amedai kuwa kwa sasa hayupo tayari kuonekana katika video ya msanii yeyote.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Mdundo’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa amechukua uamuzi huo ili kuweza kufanya zaidi kazi zake binafsi.
“Kwanza nisema tu sipo tayari kuonekana kwenye video ya msanii yeyote, iwe kwa style yoyote iwe kucheza, kuonekana tu nimeuza sura, yaani siwezi kuonekana labda kuwe na faida kubwa sana naipata,” amesema Msami.
Ameongeza kuwa kwa sasa yupo buys kufanya muziki wake na kazi ya uchezaji amewaachia watu wengine kwa sababu ameona umefika wakati wa kufanya hivyo ili na wengine wapate nafasi hiyo pia.
No comments:
Post a Comment