Friday, January 5, 2018

Asante Kwasi awazidi washambuliaji msimu huu


Mlinzi mpya wa Simba raia wa Ghana Asante Kwasi jana amefanikiwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza na klabu yake hiyo mpya kwenye michuano ya Mapinduzi na kuwazidi mabao baadhi ya washambuliaji msimu huu.

Asante Kwasi ambaye amesajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo akitokea Lipuli FC amekuwa miongoni mwa walinzi wenye uwezo mkubwa wa kufunga. Baada ya jana usiku kufunga Kwasi sasa amefikisha mabao 6 msimu huu.

Akiwa na Lipuli FC Kwasi alifanikiwa kufunga mabao 5 katika mechi 11 za ligi kuu Tanzania bara alizocheza kabla ya dirisha dogo. Asante Kwasi sasa anakaa nyuma ya Emmanuel Okwi mwenye mabao 8 katika VPL na Habibu Kiombo mwenye mabao 7 kwenye VPL.

Mlinzi huyo anayemudu nafasi ya mlinzi wa kati na pembeni kushoto alifunga bao la tatu katika ushindi wa mabao 3-1 ilioupata Simba kwenye mechi yake ya pili kwenye michuano ya Mapinduzi 2018 uwanja wa Amaan.

Pia amekuwa ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao wamefanikiwa kufunga bao katika mechi zao za kwanza na klabu mpya tena kwenye mashindano ambayo mchezaji anashiriki kwa mara ya kwanza



No comments:

Post a Comment