Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amesema kuendelea kuhama kwa Madiwani na baadhi ya wanachama wa chama hicho chanzo chake ni rushwa na sio sababu nyingine kama wao wanavyotoa.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vincent Mashinji leo kufuatia kujiuzulu kwa madiwani wawili wa CHADEMA Mkoani Iringa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Ukishakuwa kwenye nchi ambayo inaendekeza rushwa za kisiasa na kusumbua wala rushwa na mara zote mtu akishachukua mlungula ataongea kitu chochote anachokiona,maana hao waliojiuzulu jana wanasema hawaridhishwi na na CHADEMA kinavyojiongoza wao pia ni viongozi sasa mimi nashangaa lakini hapo kikubwa ni rushwa ya kisiasa ndo imewafanya kuondoka,"amesema Dkt. Mashinji.
Aidha katibu huyo wa CHADEMA ameendelea kwa kusema sio tu madiwani ambao wanafatwa na kupewa rushwa bali hata kuna wabunge na viongozi wa juu kabisa ambao wanafatwa na kushawishiwa kwa kupewa rushwa.
Mpaka sasa Manispaa ya Iringa Mjini imepoteza madiwani wa Kata sita ambao wote baada ya kujiuzulu walijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment