Friday, January 5, 2018

Aliyemuua ndugu wa Rihanna afikishwa kizimbani


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Nation News zinasema, kijana huyo anafahamika kama Shawayne Dashawn Williams ana umri wa miaka 23, amefunguliwa mashtaka ya mauaji hayo ya Alleyne ambayo yametokea wiki iliyopita katika sikukuu ya Christmas.

Shawayne alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatano hii na kesi hiyo iliahirishwa na mtuhumiwa alirudishwa gerezani huku hukumu ya kesi hiyo ikipangwa kutolewa January 31 ya mwaka huu.

Kabla ya kutokea kwa tukio hilo la mauaji, marehemu Alleyne alikuwa akitembea karibu na nyumba yake majira ya 1 usiku kabla ya kufatwa na mtu asiyefahamika na kisha kumiminiwa risasi za kutosha. Hata hivyo Alleyne alikimbizwa hospitali ya Queen Elizabeth iliyopo Bridgetown lakini alifariki dunia.

Wakati huo huo marehemu Tavon Alleyne alikuwa na Rihanna saa moja kabla ya kufariki dunia wakisherehekea pamoja sikukuu ya Christmas.



No comments:

Post a Comment