Friday, January 5, 2018

Ndoa yasababisha Manula kutokwenda Zanzibar Mapinduzi Cup


Huku michuano ya Kombe la Mapinduzi ikiendelea kisiwani Zanzibar, kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula hayupo katika kikosi hicho na anatarajiwa kufunga ndoa kesho Jumamosi.

Wakati Manula akifunga ndoa, timu yake itakuwa uwanjani kesho kuvaana na Azam FC kwenye michuano hiyo ikiwa ni mchezo wa makundi ambapo wote wapo Kundi A.

Kipa huyo alisema amefanya taratibu zote za kuomba ruhusa ili afanye namna ya kulimaliza suala hilo muhimu.

“Ni kweli sipo Zanzibar na timu kwa sababu nina ruhusa, Jumamosi ninatarajia kufunga ndoa ndiyo maana nimeshindwa kuungana na wenzangu kwa sasa kutokana na shughuli hiyo.

“Nawatakia kila la kheri wapambane na kufanya vyema, sijafahamu ni lini nitaweza kuungana na timu,” alisema Manula.

Taarifa zinaeleza, kama Simba itafika hatua za mwishoni, nusu fainali au fainali, Manula anaweza kuungana na wenzake kuipigania timu hiyo.

SOURCE: CHAMPIONI


No comments:

Post a Comment