Waziri wa Nchi ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo ameiagiza Halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini dar es salaam pamoja na Wakala wa barabara mijini na vijijini wilayani Ilala – Tarura kuhakikisha wanaanza ujenzi mara moja wa barabara ya Buguruni Mnyamani ambayo kutokana na kukithiri kwa ubovu imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kila mara.
Waziri Jaffo ametoa agizo hilo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa barabara hiyo ambapo amesema kuwa amekuwa akisikia malalamiko kutoka kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ikiwemo Channel Ten ambayo imekuwa Mstari wa mbele katika kutoa taarifa ya ubovu wa barabara hiyo.
Aidha Waziri Jaffo amepiga marufuku Ukusanyaji wa takataka jirani na kituo cha afya katika eneo hilo la mnyamani ambapo amesema katika siku za hivu karibuni ameshuhudia kupitia taarifa ya Channel Ten mlundikano wa Takataka.
Waziri Jaffo pia amekagua zahanati ya Mnyamani ambayo imekuwa ikihudumia maelfu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali lakini katika siku za hivi karibuni imekuwa ikilalamikiwa na wananchi katika utoaji huduma.
Channel Ten.
No comments:
Post a Comment