Friday, January 5, 2018

Hali ya Kingunge yaimarika


 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema hali ya mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, inaendelea kuimarika baada ya kuanza kupata matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa hospitalini hapo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Ngomuo amesema kwa sasa afya yake imeimarika.

"Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema Ngomuo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete jana Alhamisi jioni alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mwanasiasa huyo.

Kingunge aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, alifiwa na mke wake Pares Mwiru jana Alhamisi saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa.

Neema amesema mke wa mwanasiasa huyo alifikishwa Muhimbili tangu Oktoba 3, mwaka jana.

Wakati Peras akifariki,  mumewe Kingunge anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Awali mtoto wa Kingunge, Kinje Mwiru alisema kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.


No comments:

Post a Comment