Saturday, January 13, 2018
JAMANI ANTIII…NISHUSHE UNUNIO-13
ILIPOISHIA KWENYE RISASI JUMAMOSI:
“Acha mambo yako bwana, ngoja niondoke,” Vivian alisema huku akikanyaga mguu kwenye kigingi cha kukanyagia kabla ya kukaa vyema kwenye kiti cha pikipiki, ambapo yule kijana hakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kutia gia na kuondoka kwa kasi na kumuacha Bigambo akikodoa macho huku akicheka na kujisifia moyoni kwa namna ambavyo ameweza kumpata Vivian kwa urahisi na wepesi wa namna hiyo.
Kwa upande wa Vivian, kichwani alikuwa na maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu kwa wakati huo.
TEREMKA NAYO SASA…
KICHWANI aliendelea kujiuliza bila kupata majibu juu ya namna ambavyo amekuwa akiyarahisisha maisha yake kwa wanaume. Ikafika mahali akaamua kwa dhati kabisa kubadili aina na mfumo wa maisha yake yote.
“Hapana, lazima ifike mahali maisha yangu yabadilike. Haiwezekani niwe nakukuruka na wanaume kila kukicha namna hii,” Vivian alijisemea akiwa amejiinamia kwenye kiti chake. Hapohapo akachukua simu na kuamua kumpigia tena Bigambo, ili kumjulisha juu ya uamuzi wake wa kuachana na wanaume wote kwa wakati huo.
“Eeeh, Bigambo uko wapi na unafanya nini?”
“Hee, unauliza ninafanya nini kwani vipi tena na halafu ni tangu lini tukaanza kuulizana namna hiyo?” Bigambo naye akajibu kwa ukali lakini mwisho wa siku walielewana mahali pa kukutana ambapo dakika chache walikuwa pamoja waliendelea na zoezi la kugida ulabu. Kichwani mwa Vivian alishaondoa kabisa wazo la kuachana na Bigambo kama ambavyo alikuwa amedhamiria awali. Kila mmoja akaanza kuonesha ujalifu wa kupindukia kwa mwenzake.
Walianza kusimuliana jinsi ambavyo wamekuwa wakipitia kwenye changamoto nyingi za penzi lao tangu wakutane kwa mara ya kwanza kazini. Lakini Vivian alijishangaa zaidi kwa namna ambavyyo amekuwa akijisikia kuwa na penzi zito kupindukia juu ya Bigambo, mwanaume ambaye hakuwa na mazoea naye zaidi ya kukutana naye kazini tu.
Mapenzi yamekuwa yakimtesa kila mmoja wao. Vivian alimwaga siri zote na namna ambavyo huwa anajisikia raha pale anapokutana na Bigambo ambaye ameonekana ni mwanaume wa kuyaweza mambo. Kwa mara ya kwanza, Vivian alimwambia Bigambo kitu ambacho hakuwahi kukiweka wazi tangu waanza safari yao ya kutoka kimapenzi.
“Unajua ni kwa nini nilikukubalia mapema sana baaada ya wewe kunitaka kimapenzi?” Vivian alimuuliza Bigambo akiwa amemuegemea mabegani, huku mkono mmoja ukiwa kwenye glasi ya kimiminika kizito chenye rangi ya njano.
“Hapana,” Bigambo alijibu huku naye akinyanyua glasi yake na kugida maji hayo kabla ya kukunja ndita na kumtazama Vivian usoni akisubiri jibu kwa hamu kubwa sana.
“Kwenye mahusiano yangu ya nyuma sikuwahi kabisa hata siku moja kufika mwisho wa safari wakati wa mechi ya kikubwa, sanasana ni kwamba wanaume wengi hujijali wao tu kufika mwisho wa safari na kumuacha mwanamke akitapatapa njia panda, sasa wewe uliponitongoza nikajisemea ngoja nijaribu,” Vivian alisema mfululizo na kuongeza;
“Lakini tulipokutana kwa mara ya kwanza uliniweza kwelikweli, cha kushangaza nimekutana na wanaume kadhaa kwa kipindi hikihiki na sikuweza kufikia mwisho wa safari na leo ningependa sana nipate tiba tena,” Vivian alisema lakini moyoni akiwa anajiwazia ni kwa nini amekuwa mtu asiyekuwa na msimamo juu ya uamuzi wake maishani.
“Mimi huwa najali sana kumwandaa mwanamke kabla mimi sijajiandaa, unajua raha ya tendo ni mwanamke kuanza kufika mwisho wa safari ndipo ampe sapoti mwanaume, hakika hilo huwa nalizingatia sana,” alianza kujinasibu Bigambo bila kujua anaanza kumpa wakati mgumu Vivian ambaye akinywa pombe hususan Reds huwa mwepesi kushinda maharage ya Mbeya.
Hali ya Vivian ilianza kubadilika lakini alijisitiri sana asionekane kama ni dhaifu kwa kiasi hicho na pia hakuwaza kutoa penzi kwa wepesi namna hiyo ingawa Bigambo ni mwanaume wake wa siku nyingi. Kiasili, Vivian alikuwa na nyodo nyiye acheni tu. Hata huo uchangamfu aliouonesha kwa Bigambo ulitokana na ukweli kwamba jamaa alikuwa anamjulia vya kutosha.
“Kwa hiyo wewe Bigambo ni tofauti kabisa na wanaume wengi ambao hujijali wenyewe tu? Lakini mbona inakuwa hivyo?” Vivian aliuliza swali ambalo lilikuwa wazi kabisa kwa maana ya jibu lake. Kufikia hapo, hali ya Vivian ilizidi kuwa mbaya, alianza kumtazama Bigambo kwa macho yenye kulegea kama mpishi aliyezidiwa na moshi wa kuni mbichi.
“Kabisa, tena kuna wakati huwa najikuta naongeza na utaalam ambao nikiambiwa nirudie siwezi kabisa, yote hayo ni kuhakikisha najitoa ufahamu kwenye sita kwa sita, hapo sasa nitagusa na maeneo ambayo wanawake wengi huwa hawaguswi mara kwa mara,” alisema Bigambo na kuendelea;
“Unajua kuna wanawake hawajawahi kupata raha ya tendo, ukiwaaambia habari za kufika mwisho wa safari hawajui inazungumzia nini na wao wanakuambia wanafurahia mapenzi na waume zao, lakini kifupi ni kwamba hakuna mwanamke ambaye hana uwezo wa kufika mwisho wa safari, mwanamke yeyote ni maandalizi, akipata mwandaaji mzuri kabla ya mechi, ni lazima afike ukingoni tena kwa shangwe na makelele ya fujo kama siyo nderemo,” alisema Bigambo huku akisukumizia maneno hayo na glasi ya nyagi kabla hajakunja sura yake yenye mikunjo mingi kadhaa.
“Wewe B wewe jamani,” Vivian alisema na kuiweka mezani kabisa chupa ya Reds aliyokuwa ameishika mkononi, licha ya kwamba kabla hajaanza kunywa alikuwa mzima wa afya njema, awamu hii alianza kuhisi kama kuna kibaridi cha homa kali kinachoashiria malaria.
“Sasa kwa hiyo unaweza kumtibu mwanamke ambaye ana tatizo la kutofika mwisho wa safari yake?” Vivian aliuliza lakini awamu hii alishindwa kujizuia na kuuweka mkono wa kulia begani kwa Bigambo na kisha kumnong’oneza masikioni kwamba wakachukue chumba tayari kwa mazungumzo binafsi zaidi, jambo ambalo lilitoa jibu la moja kwa moja kwa Bigambo ni nini ambacho Vivian alikusudia, zaidi sana akashika glasi yenye kinywaji na kuisukumizia mdomoni.
“Eee, sana tu, mimi nimetibu sana wanawake ambao shida yao ni kutofurahia na kufika mwisho wa safari, lakini nawatibu kwa vitendo bila kufanya nao kikwelikweli,” alisema Bigambo na kuifakamia tena glasi yake ya kinywaji na kisha kumtamza usoni Vivian ambaye alikuwa kimya.
“Mmh,” Vivian aliishia kuguna na kuikamata chupa yake ya Reds.
“Vipi, mbona unaguna?”
“Mmm, kawaida tu,” alisema Vivian na kuuondoa mkono wake begani kwa Bigambo.
“Nikuombe kitu?” Vivian alianzisha tena mazungumzo.
“Sema tu Vivian.”
“Aaah, usiniite hivyo bwana,” Vivian alisema lakini sauti yake ilitoka kwa tabu na dalili za uchovu kwani pua zake zilikuwa zinabana kama mgonjwa wa mafua yenye kuambatana na malaria. Siku zote akiwa ameweka mambo yake, huwa hapendi kabisa kuitwa kwa jina la Vivian na mpenzi wake Bigambo, zaidi sana alipendelea kuitwa kwa jina la mpenzi, au sweetheart na majina mengine yenye kuashiria mapenzi.
Walinyanyuka na kwenda kuchukua chumba. Mikononi hawakuacha vinywaji vyao ambapo kila mmoja alikuwa na hamu ya kutafuna tende za mwenzake.
“Okey, samahani,” Bigambo alijitetea baada ya kumuita Vivian kwa jina.
“Bigambo nataka uwe mwanaume wangu wa kweli lakini huwezi amini nilikuwa na mawazo ya kuachana na wewe,” Vivian alisema na kumtazama tena usoni Bigambo lakini pia akawa kama anayesikilizia jibu ambalo hakujua lingetokaje kwa wakati huo. Tayari walishaingia chumbani na kukaa kitandani ambapo walisogeza meza iliyokuwa chumbani humo na kuweka vinywaji vyao.
Hata hivyo, kabla Bigambo hajasema chochote kutokana na kauli ya Vivian alimimina tena nyagi kwenye glasi na kuipiga yote kabla ya kumimina tena na kuiweka mezani bila kuinywa na hapohapo akanyanyuka kidogo na kukiweka sawa ambapo sasa aligeukiana na Vivian, alimtazama usoni na wote wakawa wametazamana bila kupepesa macho na Bigambo akapanua mdomo kama anayetaka kuuliza kitu kwa staili ya kipekee.
“Sawa, tuendelee kuwa kwenye mahusiano na mimi kukufurahisha wewe ni sehemu ya kazi yangu,” Bigambo alisema huku akikamata glasi na kujimiminia kwa kasi huku akikunja ndita, uchungu wa nyagi uliendelea kulipa kazi ya ziada koromeo lake.
Vivian alikaa kimya kwa muda. Kabla hajasema lolote, alikamata chupa ya Reds na kujimiminia kama alivyofanya Bigambo. Walikaa kimya kwa muda kabla ya kuendelea na mazungumzo.
Kuona kama Bigambo anamchelewesha, Vivian alimsogelea na kuanza kumpa uchokozi wa wazi kabisa ulioashiria kwamba anataka dozi ya maana kwa wakati huo na siyo maneno mengi kama ilivyokuwa wakati wakiwa nje.
“Baby,” Vivian aliita kwa sauti kavu lakini yenye kuelemewa na mahaba mazito sana.
“Mmmh,” Bigambo aliitika lakini kabla hajafanya chochote alishangaa kumuona Vivian akichukua nguo na kuanza kuvaa huku akitokwa na machozi.
Je, nini kitafuata? Usikose kufuatilia Siku ya Jumamosi kwenye Gazeti la Risasi0673 42 38 45 (tuma sms tu).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment