Thursday, January 4, 2018
Kikwete ampa pongezi Fid Q
Mbunge wa Chalinze (CCM) Ridhiwani Kikwete amempongeza Fid Q baada ya kutii kauli ya Rais John Pombe Magufuli ambayo aliitoa Jumanne Disemba 12, 2017 kwenye Kamati Kuu ya CCM na kuwataka wasanii wa kike kuvaa vizuri kwenye video zao.
Ridhiwani Kikwete ametoa pongezi hizo baada ya kuiona video mpya ya Fid Q anayokwenda kwa jina la 'Fresh Remix' ambayo ndani yake mabinti wengi ambao wameonekana kwenye video hiyo walikuwa wamevalia magauni marefu ambayo yameonekana kuwasitili na kuwapendeza zaidi bila kuharibu muonekana wa video hiyo.
"Hii inaitwa tii bila shuruti. Hongera sana mdogo wangu Diamond, Fid Q kwa kuonyesha usikivu. Mavazi mazuri ni yale yanayohifadhi utu na jinsi. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" aliandika Ridhiwani Kikwete
Rais Magufuli akiwa kwenye Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM mwaka jana Disemba 12 aliwataka Jumuiya ya Wazazi ya CCM kutokaa kimya pindi wanapoona mambo mabaya katika jamii na alisema kuwa amekuwa akikerwa na tabia ya baadhi ya wanawake kwenye video za wasanii wa bongo kuvaa vibaya na kuonyesha maumbile yao ya ndani kitu ambacho hakikubaliki.
Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli wasanii hawa wakubwa wamenza kuwa mfano kwa kuwavalisha wapambaji wa video yao nguo ndefu ambazo zimesaidia kuipamba video hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment