Friday, January 5, 2018

Vijue Vipimo Vinavyotumika Kupima Kama Una Vidonda Vya Tumbo



Miongoni mwa magonjwa ambayo yanawasumbua watu wengi sana ni pamoja na vidonda vya tumbo hivyo, Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha una  vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-

1.   Kupima damu 'Blood test'
Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

2.   Kupima pumzi 'Breath test'
Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

3.   Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'
Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi.  Vilevule kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

4.   X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'
Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

No comments:

Post a Comment