Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule ambaye ni Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, amechukua uamuzi wa kuua familia yake kutokana na wivu wa mapenzi.
Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Benedict Kitalika amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kusema kuwa muuaji alifanya tukio hilo usiku wa jana huko nyumbani kwao Kimara jijini Dar es salaam, na kisha kutokomea kusikojulikana.
“Ni kweli mwanaume mmoja ambaye anafanya kazi ya uhasibu katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule, ameua mke, mtoto na shemeji yake, inasemekana kulikuwa na ugomvi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa huyu mtoto mdogo sio wake na anajihusisha na mapenzi na wanaume wengine, hivyo aliamua kuwaua kwa jembe na kukimbia”, amesema Kamanda Kitalika.
Kamanda Kitalika ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo marehemu aliacha ujumbe kuwa polisi wasihangaike kwani yeye ndiye kafanya mauaji.
Jeshi la Polisis limesema taarifa za tukio hilo walizipata kutoka kwa majirani baada ya kugundua hakuna dalili ya kuwepo watu kwenye hiyo nyumba na kuanza kuchunguza, ndipo walipogundua hayo na kuita polisi kuvuja mlango.
Waliouawa kwenye tukio hilo wametajwa kuwa ni Upendo Lukule ambaye ndiye mke, Magreth Samuel ambaye ni shemeji mtu na mtoto mdogo ambaye umri wake ni chini ya mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment