Wednesday, January 3, 2018

Trump afunguka kuhusu Marekani kumiliki silaha za Nyuklia


Rais wa Marekani, Donald Trump leo ameuthibitishia ulimwengu kuwa hata Marekani inamiliki silaha za Nyuklia ingawaje imekuwa mstari wa mbele kupiga vita utengenezwaji wa silaha hizo kwa mataifa mengine duniani.

Haya yamethibishwa na Rais Donald Trump baada ya kumjibu Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jung Un kwa kauli yake aliyoitoa wiki iliyopita akioonya Marekani kuwa kitufe cha kuwashia makombora yake kipo kwenye kitanda chake akimaanisha kuwa muda wowote anaweza kuilipua Marekani.

Trump naye kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa hata yeye ana kitufe cha kuwashia makombora ya silaha za nyuklia na kumuonya kwa kumwambia kuwa silaha zake ni kubwa kuliko za Korea Kaskazini.

Rais huyo ambaye haishiwi vituko ameongeza kwa kusema kuwa Rais Kim amekuwa mbwatukaji wa kutoa vitisho kila siku lakini hakuna chochote na kumuonya kwamba yeye kitufe chake kinafanya kazi.

“Kiongozi wa Korea Kaskazini ameanza kuongea tena “nina kitufe cha nyuklia kwenye meza yangu” kama siku zote huwa anavyosema. Sasa nawaomba mmwambie huyo mlafi kuwa hata mimi nina kitufe cha silaha za nyuklia tena kubwa kuliko za kwake, na kitufe changu kinafanya kazi.”ameandika Rais Trump.



No comments:

Post a Comment