Friday, January 5, 2018

Umuhimu wa Kujiongeza katika maisha ya mafanikio



Habari za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, ni matumaini yetu mazima u mzima wa afya tele na unaendelea vyema katika harakati zako za kuweza kulisukuma gurudumu hili la maendeleo.  Ni siku nyingine tulivu ambayo sina budi nikukaribishe kwa moyo mkunjufu tuweze kujifunza kwa pamoja.

Siku ya leo nataka ttuzungumzie namna ambayo una uwezo mwingine wa kutenda jamno jingine ambalo linaweza kukupa mafanikio makubwa kwa upande wako tofati na hilo ulitendalo sasa. Unajua nataka tuzungumzie hili kwa sababu wetu wengi hawafahamu uwezo mwingine walionao, ambao unaweza kuutumia ili uweze kukamilisha jambo jingine ambalo Mwenyezi mungu kakujalia kiulitenda.

Watu wengi hudhani ya kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa kufanya. Kwa mfano mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea kitu fulani, basi baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka mipaka katika kitu hicho pekee.

Ukweli haipo hivyo hata chembe, kwani kila binadamu binadamu kaumbwa  na uwezo mwingine wa kufanya vitu vingi ambavyo vitaweza kumuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya kimafanikio. Hata kanuni ya kufanya mazoezi ya mwili inasema ya kwamba huwezi kutengeneza six park kwa kufanya mazoezi ya aina moja pekee kila wakati, bali unaweza kutengeza six park kwa kufanya mazoezi ya aina tofauti tofauti.

Kwa  muktadha huo kama kweli unataka kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa, unachotakiwa kufanya ni kuweza kutambua uwezo mwingine ambao mwenyezi Mungu kakuwekea ndani yako, ili uweze kujipatia mkate wako wa kila siku.

Hata mwandishi mmoja aitwaye Antony Robbison aliwahi kuandika ya kwamba “if you do what you have done you will get what you always gotten” hii ikiwa na maana “kama utafanya mambo yaleyale ambayo umekuwa  ukifanya siku zote, utapata yale yele ambayo siku zote umeyapata”. Naomba urudie kusoma tena aya hii ili uielewe vizuri.

Kwani aya hiyo ipo wazi kabisa kama umezoea kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile basi matokeo yake, yatakuwa ni yaleyale. Hivyo ili uweze kupata matokeo ya iana tofauti  na uliyoyazoea, unachotakiwa kufanya kubomoa uzio wako wa kufikiri kwa kuanza kubadili ratiba ya kutenda mambo yako ya msingi. Lakini pia ongeza uzio wa kufanya mambo yako  kwani binafsi naamini una kitu kingine cha kufanya zaidi ya hicho ambacho unakifanya.

Mwisho nimalizie makala haya kwa kusema ukitaka kwenda mbali zaidi katika mambo yako ya msingi acha kujenga uzio ambao utakufanya ushindwe kuona fursa nyingine,  bali unachotakiwa kufanya ni kubomoa uzio huo ili uweze kuona fursa mbalimbali ambazo zimejificha, kwani pindi unavyoacha ukuta huo ni kule kutengeneza uwezo wako wa kulalamika, na mwisho wa siku kuelekea jehenamu ya umasikini.

Narudia kwa kusema tena pale unaposhindwa kujiongeza ni kutengeneza jehanamu ya umaskini. Usiogope na kusema afisa mipango anakutisha hapana,  ila kazi yangu ni  kukwambia ukweli ambao upo wazi, kwani nafasi uliyonayo sasa unachotakiwa kufanya ni kuwaza ni namna gani utaweza kufika mbali zaidi.

Kwani umuhimu wa kujiongeza kunamsaidia mtu kuweza kuwa milango mingi ya kuweza kufanikiwa zaidi. Pia faida nyingine ya kujiongeza humsaidia mtu kuweza mbunifu zaidi kwa kile akifanyacho. Na ubunifu humsaidia mtu aweze kujilikana na ukijulikana ndo mwanzo wa mafaniko yenyewe. Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba kazi ibaki kuwa kwako kwa kuamua kwenda kuyatekeleza hayo ambayo nimekwambia. Asante.Ni wako katika ujenzi wa mafaniko; afisa mipango Benson Chonya


No comments:

Post a Comment