Friday, January 5, 2018

Agness afunguka penzi la Rammy


MUUZA nyago machachari Bongo, Agness Mmasi amesema kuwa, kamwe hawezi kulisahau penzi la msanii wa filamu Bongo, Rammy Gallis, sababu ana mahaba mazito na mwanaume huyo.

Akipiga stori na Star Mix msanii huyo ambaye ana orodha kubwa ya kubanjuka na mastaa alisema, katika wasanii wote aliowahi kuwa nao, mwanaume anayempenda sana ni Rammy na ni ngumu kwake kusahau penzi lake sababu anatambua thamani ya mwanamke.

“Nampenda sana Rammy japo nilishapita lakini ni ngumu kumsahau, halafu ni mwanaume ambaye muda wowote akinihitaji siwezi kumringia sababu bado namzimia vibaya, naweza kusema ndo’ msanii pekee katika wale niliowahi kuwa nao ambaye ananihe-shimu, ”alisema.


No comments:

Post a Comment