MTANGAZAJI wa Runinga ya Magic Swahili kupitia kipindi cha Harusi Yetu, Penniel Mungilwa ‘Penny’amefunguka kuwa, kuna uwezekano alikuwa na gundu la kutoolewa mwaka 2017 lakini anaamini mwaka huu, 2018 ataolewa kwa uwezo wa Mungu.
Akizungumza na gazeti hili, Penny alisema mwaka huu yuko tayari kwa ndoa na kwa mwanaume sahihi kwani ameomba vya kutosha.
“Mwaka huu ni wa baraka kwangu na gundu nyingi zimeshaondoka 2017, mwaka huu kwangu ishallah shela litakaa mwilini mwangu, mwanaume yupo tayari,” alisema Penny bila kumtaja jina mwanaume wake.
No comments:
Post a Comment