Thursday, January 4, 2018

Rais Magufuli apata ujumbe kutoka kwa Museveni



 Rais wa Uganda Kaguta Museveni leo Januari 4, 2018 amemuandikia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumpa salamu za mwaka mpya pamoja na kuzungumza juu ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Ujumbe huo wa Rais Museveni umewasilishwa Ikulu ya jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Sam Kutesa ambapo pia Waziri huyo amefanya mazungumzo na Rais Magufuli.

Mara kadhaa Rais Magufuli na Museveni wamekuwa wakinukuliwa wakisema kuwa Uganda na Tanzania ni ndugu jambo ambalo limepelekea nchi hizi mbili kuwa na ushirikiano wa karibu na kuchochea maendeleo ya nchi zote mbili kwa miradi mbalimbali ambayo imeanza ikiwepo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.



No comments:

Post a Comment