Msanii wa muziki wa Dansi hapa nchini Christian Bella amefunguka na kupangua kashfa ya dawa za kulevya iliyosambazwa mitandaoni na kusema kwamba wanaosambaza taarifa hizo ni watu wenye chuki binafsi na pia hawezi kumlaumu msambazaji wa taarifa hizo.
Akizungumzia stori hiyo, Bella amesema kwamba hawezi kujiingiza kwenye starehe ya dawa za kulevya kwani anaelewa ni nini mwisho wake na huku anajijua majukumu aliyo nayo.
Akizidi kupangua tuhuma hizo, Bella amesema kwamba "Mimi ni baba, nina familia kubwa sana na majukumu pia siwezi kujiingiza kwenye starehe hizo za vijana japo mimi ni kijana. Najua ni watu wenye chuki na mimi ndiyo wanasambaza uzushi huo lakini siwezi kumlaumu wala kuumia kwani najua nilipotoka. nilishakatishwa sana tamaa mpaka nimefika hapa na ninajijua nina maadui mengi hivyo sijashtuka sana na habari hizo".Amesema Bella
Pamoja na hayo Bella ameongeza kwa kuwaambia mashabiki zake kwamba hawezi kuja kuiingia kweye matumizi ya dawa za kulevya na kuweka bayana kwamba ni kweli alishindwa kufanya 'show' mbili zinazozungumziwa kwa sababu alikuwa amelazwa na siyo uteja kama ilivyozushwa.
Mapema wiki hiii habari za kuhusu Msanii Christian Bella kutumia dawa za kulevya ziliibuka na kuwafanya mashabiki wa msanii huyo kushikwa na simanzi.
No comments:
Post a Comment