Thursday, January 4, 2018
Msuva atua nchini, aelezea ugumu wa Ligi ya Morocco
Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva wa Difaa El Jadida, amewasili asubuhi ya leo Alhamisi kwa mapumziko mafupi baada ya Ligi Kuu Morocco 'Batola Pro' kusimama kwa muda.
Msuva ameifungia Difaa mabao matano kwenye michezo 14 kati 15 ambayo ameichezea timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza wa Batola Pro ambao umemalizika.
"Nitakitumia kipindi hiki cha mapumziko mafupi kwa kuwa karibu na familia yangu, nitakuwa hapa kwa wiki moja na baada ya hapo nitarejea Morocco," amesema mchezaji huyo wa zamani wa Yanga.
Hata hivyo Msuva amekiri kuendelea kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano kutokana na wakazi wengi wa nchi hiyo kuzungumza Kiarabu na Kifaransa.
"Haiwezi kuwa haraka hivyo, itanichukua muda kuanza kuzungumza vizuri lugha zao japo kwa sasa kuna baadhi ya maneno yao mepesi nimejifunza," amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment