Mwanaume mmoja nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Boniface Okwero anaripotiwa kujiua baada ya kupikiwa majani ya kunde na mkewe kama mlo wa siku ya Mwaka Mpya.
Okwero ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nanyungu Emauko inaelezwa kuwa aliporudi nyumbani kutoka kwenye mizunguko yake siku hiyo ya Mwaka Mpya na kukuta majani ya kunde, uliibuka ugomvi mkubwa baina yao huku akimuuliza mkewe kwanini hajapika nyama au kuku kama mlo wa sikukuu.
Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Boniface Oyosa, baada ya mzozo huo mkubwa, marehemu aliichoma nyumba yao moto ambayo alikuwa akiishi na mkewe huyo na baadaye kujiua. Aliongezea kuwa mwanamke alipika chakula hicho kwasababu hakuwa ameachiwa pesa ya kutosha kununua na kupika kuku au nyama.
No comments:
Post a Comment