Thursday, January 4, 2018

Yanga yaiduwaza JKU. Kessy aibuka shujaa


Yanga imeinyoosha  JKU kwa kuichapa kwa bao 1-0 lililofungwa na katika dakika ya 89 katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar.

Huu unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo wa Yanga katika michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi.

Bao la Yanga limefungwa katika dakika hizo za mwishoni na beki Hassan Kessy ambaye alianzisha mashambulizi kabla ya kumalizia kazi hiyo.

Kessy amekuwa shujaa wa Yanga kwa kufunga bao hilo wakati timu hizo zilionekana kama zinaenda sare ya bila kufungana.

Kabla ya mchezo huo, Singida United iliendeleza ushindi kwa kuitwanga Taifa ya Jang’ombe kwa mabao 3-1.



No comments:

Post a Comment