MUUZA nyago machachari Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ anadaiwa kupokonywa gari aina ya Subaru na mwandani wake ambaye ni kigogo wa serikali baada ya kushindwana tabia.
Taarifa kutoka kwa chanzo kilicho karibu na mrembo huyo zimeeleza kuwa, bishosti huyo licha ya kujitapa kwamba gari hilo alinunua mwenyewe, ukweli ni kwamba alipewa na bwana’ke ambaye alikuwa anaishi naye kinyumba maeneo ya Tabata jijini Dar.
“Ile gari Kidoa alipewa na huyo mwanaume wake, sasa kuna mambo walishindwana kwenye uhusiano wao ikabidi kila mmoja asepe kivyake, ndipo yule jamaa akampokonya gari,”kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, paparazi wetu alimtafuta waya Kidoa, akafunguka.
“Ni kweli sionekani na gari mjini, kuna siku nilipata ajali mbaya niligongana na basi, hivyo lipo gereji linaendelea na matengenezo, soon mtaliona.”
No comments:
Post a Comment