Kim Kardashian na mumewe Kanye West wameamua kuuanza mwaka 2018 kwa kuhamia katika mjengo wao ambao waliukimbia kwa zaidi ya miaka mitatu.
Wawili hao wanadaiwa kuwa walitumia kiasi cha dola milioni 20 kununua nyumba hiyo iliyopo huko Hidden Hills kutoka kwa mwanamuziki Lisa Marie Presley ambae ni mtoto wa pekee wa muigizaji Elvis Presley.
Wapenzi hao walinunua mjengo huo wa kifahari tangu mwaka 2014 kwa kiasi hicho ambapo mpaka sasa baada ya kuufanyia matengenezo unatajwa umefikia kuwa na thamani ya kiasi cha dola milioni 60.
Kim na Kanye walimwaga mapesa hayo mengi kuununua mjengo huo ambapo tayari wamehamia na watoto wao, pia wametumia zaidi ya dola milioni 20 katika kuufanyia marekebisho japo mpaka sasa haujamalizika kabisa.
Katika mjengo huo pia kuna chumba maalum kwa ajili ya mambo yote ya muziki ambapo umechukuwa sehemu kubwa ya maisha ya Kanye.
No comments:
Post a Comment