Thursday, January 4, 2018

Wakulima wa korosho mkoa wa Pwani wapewa ushauri wa bure kuhusu kuchelewa malipo


Na. Ahmad Mmow, Dar
KATIKA  kuhakikisha wakulima wote wa korosho wa mkoa wa Pwani ambao hadi sasa hawajalipwa fedha zao wanalipwa. Wameshauri kutekeleza maagizo na ushauri wa wataalamu na wanunuzi wa zao hilo.

Wito huo ulitolewa jana na mwenyekiti wa chama kikuu cha cha ushirika cha CORECU, Rajab Ng'onoma alipozungumza na Muungwana ofisini kwake mjini Kibaha.

Ng'onoma ambae alitoa ushauri huo kufuatia malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wakulima  wa korosho mkoani humo kutolipwa fedha zao, alisema wakulima hawana budi kukubali na kutekeleza masharti na maelekezo na ushauri unaotolewa na wataalamu na wanunuzi kuhusu ubora wa korosho zao. Badala ya kubishana nao.

Alisema sababu ya baadhi ya wakulima kutolipwa nikutokana na korosho zao kutokuwa na ubora ambao wanunuzi walitarajia. Hivyo wanunuzi hao kugoma kununua.

Alisema wanunuzi waliomba kununua korosho za daraja la kwanza, hata hivyo baadhi ya korosho hazina ubora hata wa kiwango cha daraja la pili. Hali inayosavabisha korosho hizo kushindwa kununuliwa na zinaendelea kusota maghalani.

"Tatizo hilo halipo kwa wakulima wa Mahege pekee bali maeneo mengi tu. Kwenye chama changu cha msingi cha Lukangawadi kina tani takribni 116 hazijanunuliwa. Tayari tumeanza kuzichagua na kuanika kama wanavyotushauri wataalamu. Ila wengine hawataki, wanaona watapunguza uzito na wengi wa korosho zao. Matokeo yake wanunuzi hawanunui na wao hawapati fedha, "alisema Ng'onoma.

Mwenyekiti huyo Alibainisha kwamba sababu kubwa ya kutonunuliwa korosho hizo nikukosa ubora nasio wafanyabiashara.

Ununuzi unaoendelea, wakubali kuanika, wao wenye mali niwakulima wenyewe. Hatuwezi kuwalazimisha, lakini nawafanya biashara hawawezi kununua korosho rijekti (zisizo na ubora) matokeo yake ni malalamiko hayo, "alisema kwa masikitiko Ng'onoma.

Alisema sababu za korosho nyingi kuwachafuka ni mvua zilizonyesha mkoani humo wakati korosho zikiwa mashambani. Hata hivyo njia pekee ya kuzirejesha kwenye ubora ni kuanika na kuchagua. Hata hivyo wakulima wengi hawataki, wanaamini watapunguza uzito na wengi.

Licha ya wito huo, mwenyekiti huyo alitoa wito kwa wakulima wa zao hilo mkoani humo kuthamini zao hilo kwa kufanyia palizi na usafi badala ya kuvuna zikiwa kwenye majini. Kwani miongoni mwa sababu za korosho kuchafuka nikudondokea kwenye majani. Huku akibainisha kwamba iwapo mashamba yangekuwa safi kusingekuwa na madhara hata kama zilinyeshewa mvua.

Mikorosho mingi niyaurithi, imezeeka, tupande mikorosho mipya nayakisasa. Mikoa mingine imeanza imeanza kuzalisha korosho, tukiendelea na hali hii tutaachwa na tukuwa vibarua kwao, "alitahadharisha Ng'onoma.

Maelezo ya Ng'onoma yalishabihiana na maelezo ya diwani wa kata ya Mahege, Hamisi Mamba na katibu wa chama cha msingi cha ushirika cha Mahege, Sada Kiyungi ambao nao walisema miongoni mwa sababu za baadhi ya wakulima kutolipwa ni Moro's go zao kutonunuliwa kutokana na kukosa ubora.

Awali baadhi ya wakulima waliopeleka korosho zao katika chama cha msingi cha Mahege, walisema hawajalipwa hadi sasa. wakulima hao waliozungumza na Muungwana mwanzoni mwa wiki hii, walisema baadhi yao waliopeleka kwenye maghala ya vyama vya msingi tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Hata hivyo hadi sasa hawajalipwa nahawajui watalipwa lini.



No comments:

Post a Comment