Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo imetenga zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya uboreshaji wa Zahanati ya Kimara manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam huku pia ikiwataka wakurugenzi kuhakikisha fedha za dawa zinatumika kama ilivyopangwa.
Hayo ameyasema katika ziara yake ya siku moja ndani ya manispaa ya Ubungo Dar es Salaam.
Waziri Jafo amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni mia saba ambapo milioni mia nne kati yake inalenga kujenga jengo la kituo cha afya cha Kimara huku milioni mia tatu zikitengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba lengo ikiwa kuboresha huduma za afya ndani ya manispaa hiyo.
Waziri Jafo akiwa manispaa ya Ubungo alitembelea soko la Mabibo ambapo huku kero kuu ilikuwa ni tozo kubwa wanazotozwa wafanyabiashara licha ya marufuku ya serikali ya kubeba Lumbesa ambapo katika kituo cha afya cha Kimara wananchi walisema ukosefu wa dawa ni moja ya changamoto zinazowakabili.
Uongozi wa manispaa ya Ubungo umesema utahakikisha unasimamia kikamilifu maagizo yote ya seriklai ikiwa ni pamoja na usimamiaji wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kimara ili kikamilike haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment