Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kanyara wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kwa kukutwa na nyara mbalimbali za serikali, yakiwemo magamba 40 ya mnyama aina ya Kakakuona na vipande vitatu vya nyama ya Simba.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishna Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Ngerezya Chamukaga ambaye alikamatwa desemba 21 majira ya saa moja usiku akiwa na nyara za serikali kama anavyozitaja kamanda huyo wa polisi mkoani hapa.
Katika hatua nyingine, mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Kamishna msaidizi wa polisi Mukadam Mukadamu ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi jijini Mwanza, ambapo mabasi matatu yanayosafirisha abiria kuelekea jijini Dar es Salaam yamezuiliwa.
Baadhi ya madereva wa mabasi yaliyofanyiwa ukaguzi wa leseni na kuwapima kilevi, wameupongeza utaratibu huo na kuomba uwe endelevu, huku abiria pamoja na wadau wengine wa usafiri wakisema ukaguzi huo wa kushtukiza unawafanya madereva wengi kuwa makini pindi wanapokuwa safarini na hivyo kupunguza ajali za mara kwa mara
No comments:
Post a Comment