Monday, January 1, 2018

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kubaka watoto tisa



Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara,limemkamata mwalimu mmoja wa shule ya msingi ya Itiryo wilayani humo Bw Samwel Mariba Daniel mwenye umri wa miaka ishirini kwa kutuhuma za kuwabaka wanafunzi tisa wenye umri kati ya miaka saba hadi miaka tisa.

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Jeshi la polisi Henry Mwaibambe,amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mwalimu huyo wakati akijiandaa kutoroka kwenda nchi jirani ya Kenya.

Akizungumzia oparesheni ambayo inaendeshwa hivi sasa ya kupambana na biashara na kilimo cha zao haramu la bangi,kamanda huyo wa polisi kanda hiyo maalum ya Tarime na Rorya,amesema jeshi hilo limefanikiwa kukamata pikipiki nne zilizokuwa zikisafirisha shehena ya bangi kwenda nje ya nchi.

Hata hivyo kuhusu tatizo kubwa la wizi wa mifugo katika kanda hiyo maalum,Kamanda huyo wa Jeshi la polisi,amesema kuwa makachero wa Jeshi la Polisi wamefanikiwa kudhibiti wizi wa mifugo baada ya kubaini maeneo maalum yanatumika kuficha mifugo baada ya kuibwa.

No comments:

Post a Comment