Monday, January 1, 2018

Johari aamua kuokoka


MWIGIZAJI ‘mhenga’ Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amedai kubadili mfumo wa maisha yake na kuahidi kuokoka ili kujiweka karibu na Mungu, ikiwa ni pamoja na kuachana na maisha ya ajabu kama matumizi ya pombe.

Johari aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, amebaini maisha ni mafupi duniani hivyo ni vyema kujisafishia njia na kumrudia Mungu ambaye ndiye mwokozi wa maisha ya wanadamu.

“Ninaachana kabisa na mambo ya kidunia, sitaki tena pombe wala kujihusisha na maisha mengine yenye kumchukiza Mungu, nimefanya mambo mengi yasiyokuwa mazuri. Kama binadamu, ninajipanga kuwa mpya na ninasema kabisa kwamba nimeokoka,” alisema Johari.



No comments:

Post a Comment