Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka vijana kuchangamkia kilimo cha korosho kwani zao ambalo kwa sasa lina fursa nyingi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji wa Mikorosho Bora na mipya iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
"Mahitaji ya korosho ni makubwa duniani, korosho zinatumika mahotelini na kwenye mikutano mikubwa, zinatumika kwenye ndege, kwa hiyo bei yake lazima iwe kubwa”amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
No comments:
Post a Comment