Monday, January 1, 2018

Masoud Kipanya awatoa hofu watanzania





KUFUATI taarifa kusambaa mitandaoni jioni ya leo Januari 1,2018 kwamba, mchora katuni maarufu Tanzania, Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi, Kipanya kupitia akaunti yake ya Twitter ameibuka na kuwatoa hofu Watanznia kwa kuandika kauli hii.
“Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.”
Taarifa hizo zinadai kuwa, Masoud Kipanya ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds FM, amekamatwa na Polisi baada ya kuchora katuni ambayo ina maudhi ya uchochezi kati ya wananchi na serikali. Aidha katika kauli yake Masoud hajaweka wazi iwapo amekamatwa na amepelekwa kituo kipi cha polisi na kama ameachiwa au bado.

Soma Zaidi Hapa

No comments:

Post a Comment