Sunday, December 31, 2017

Rais Karia aguswa na msiba wa Mwandishi



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mtangazaji wa Kituo cha Radio Uhuru, Limonga Justin Limonga.

Msiba huo wa mwanahabari mwandamizi umetokea leo Desemba 31, 2017 kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kutokana na msiba huo, Rais Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Radio, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) pamoja na wanafamilia wote wa mpira wa miguu.

''Natambua mchango wa Limonga katika kupasha habari za michezo kupitia Radio'', amesema Karia.

Aidha Karia ameongeza kuwa hatuna budi kuwa na imani kama maandiko yanavyosema kwamba Bwana ametoa na bwana  ametwaa jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment