Friday, December 29, 2017

Omog apata dili la kuinoa El-Merreikh





Siku chache baada ya kufungashiwa virago na Klabu ya Simba, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog amepata dili nchini Sudan.

Omog ambaye hivi karibuni alifungashiwa virago na Simba kutokana na kushindwa kuiongoza timu hiyo kupata matokeo mazuri katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Green Warriors amepata dili katika Klabu ya Al-Merreikh ambayo ni moja kati ya miamba ya soka nchini Sudan.

Juzi Jumatano, Al-Merreikh ilimtumia barua pepe Omog ya kumtaka akajiunge na timu hiyo kutokana na kuvutiwa na utendaji wake wa kazi wakati alipokuwa akiitumikia Simba lakini pia wasifu wake alionao katika soka la Afrika.

Habari za kuaminika zinaeleza inadaiwa kuwa baada ya barua hiyo Omog aliwajibu na kuwataka wampatie muda wa mwezi mmoja ili aweze kwenda kwao Cameroon na kuweka mambo yake sawa.

“Omog anatarajia kuondoka nchini Jumamosi endapo atamalizana na uongozi, lakini jana (juzi) amepokea barua pepe kutoka Sudan katika Klabu ya Al-Merreikh ikimhitaji akawe kocha mkuu wa timu hiyo.

“Hata hivyo, aliijibu barua hiyo na kuwaambia wampatie muda kwanza aende kwao akaweke mambo yake sawa,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza:

“Pia ukiachana na dili hilo, huko kwao nao wamemuita ili akakabidhiwe majukumu katika timu yao ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON ya mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment