Korea Kaskazini katika salamu zake za mwisho wa mwaka imesema haitoachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ikiwa Marekani na washirika wake wataendelea kufanya mazoezi ya kijeshi karibu na nchi yake.
Shirika la habari la Korea Kaskazini limetoa taarifa hiyo leo katika uchambuzi wake kuhusu silaha kubwa za kinyuklia zinazomilikiwa na taifa hilo pamoja na majaribio ya makombora yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo katika mwaka huu 2017.
Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake kubwa la makombora mnamo mwezi Septemba na katika miezi ya Julai na Novemba ilizindua makombora matatu yenye uwezo wa kuruka kutoka bara moja hadi jingine.
Uzinduzi huo ulizusha wasiwasi kwamba huenda nchi hiyo ikawa inamiliki bomu la kinyulia linaloweza kurushwa hadi nchini Marekani na hivy kuitia hofu Marekani na kuchukua hatua za kuiwekea vikwavyo vipya katika Baraza la Uslama la Umoja wa mataifa.
No comments:
Post a Comment